ELON MUSK AZINDUA XCHAT, APP MPYA INAYOENDA KUSHINDANA NA WHATSAPP NA TELEGRAM
Elon Musk kupitia kampuni ya X Corp. amezindua rasmi XChat, app mpya ya mawasiliano inayolenga kuingia moja kwa moja kwenye ushindani dhidi ya WhatsApp, Telegram pamoja na apps nyingine kubwa za chatting. Taarifa zinaonesha kuwa XChat imeanza kupatikana kwa watumiaji wa iPhone na iPad, huku watumiaji wa Android wakisubiri uzinduzi wake rasmi.
XChat ni sehemu ya mpango mkubwa wa Elon Musk wa kuifanya X kuwa “everything app”, yaani app moja yenye huduma nyingi kama mawasiliano, mitandao ya kijamii, biashara na huduma nyingine za kidigitali.
Kwa wale waotumia iphone unaweza kuipata app uko appstore ila kwa watumia wa android Twendelee kusubiri pia tutapeana Updates.
SIFA KUBWA ZA XCHAT
1. Kutuma ujumbe binafsi na group chats kwa mfumo wa kisasa.
2. Audio calls na video calls ndani ya app.
3. Kushare mafaili kwa urahisi.
4. Uwezo wa kuedit message baada ya kutuma.
5. Disappearing messages kwa mazungumzo ya faragha.
6. Screenshot blocking kwenye baadhi ya chats.
7. Mfumo wa kutumia account ya X badala ya kutegemea namba ya simu pekee.
XCHAT ITATOFUTIANAJE NA WHATSAPP?
WhatsApp imezoeleka zaidi duniani kutokana na idadi kubwa ya watumiaji, calls zenye ubora pamoja na matumizi rahisi kwa familia na biashara.
XChat kwa upande wake inaleta mfumo mpya unaounganishwa moja kwa moja na X, jambo linaloweza kuwavutia watu wanaotumia mtandao huo kila siku.
XCHAT ITATOFUTIANAJE NA TELEGRAM?
Telegram inajulikana kwa groups kubwa, channels na bots.
XChat inalenga simplicity, privacy features pamoja na kutumia nguvu ya brand ya X yenye mamilioni ya watumiaji duniani.
JE XCHAT INAWEZA KUFANIKIWA?
Nguvu ya jina la Elon Musk, umaarufu wa X na hamasa ya watu kupenda apps mpya vinaweza kuifanya XChat kupata watumiaji wengi kwa haraka. Hata hivyo, bado itahitaji muda kujenga trust, stability na kushindana na apps zilizokaa sokoni kwa miaka mingi.
Kwa maoni yako, XChat inaweza kuitikisa WhatsApp na Telegram au itabaki kuwa app ya wapenzi wa X pekee?


Wa kwanza kuweka comment
ReplyDelete