Upatikanaji na utumiaji wa ‘SHAKTech143‘ ndani na nje ya Tanzania unawezeshwa
na SHAKTech143 (watumiaji wa kimataifa na kitaifa wanaweza kutupata katika mitandao ya kijamii, kwa masharti yafuatayo:
1. Kwa kutumia SHAKTech143‘
unakubaliana na kanuni hizi, ambazo zinaanza kutumika mara tu unapoanza kuingia SHAKTech143‘. Endapo haukubaliani na yote tafadhali usiingie, kutumia na /au
kuchangia katika majukwa ya SHAKTech143‘.
2. SHAKTech143 inaweza kubadilisha masharti haya
mara kwa mara kwa hiyo zingatia na kufatilia mara kwa mara. Utumiaji wako wa SHAKTech143‘
utachukuliwa kuwa kukubaliana na masharti yaliyoongezwa au kubadilishwa. Endapo
haukubaliani, unatakiwa kuacha kutumia tovuti hii. Endapo kuna mgongano wowote
kati ya masharti haya na masharti yanaweza kuonekana sehemu nyingine za SHAKTech143‘ (ikiwa ni pamoja na taratibu za kurasa) hivyo kwa mapya na yanayohusika zaidi
yatatumika.
Utumiaji
1. Unakubali kwa kutumia SHAKTech143‘ kwa shughuli zinazokubalika kisheria, na vyovyote vile
isizuie haki, kukataza mtu yoyote kutumia na kufaidi SHAKTech143‘.
2. Mambo
yanayokatazwa ni pamoja na unyanyasaji au kusababisha tabu au usumbufu kwa mtu
yoyote, kusambaza maudhui yenye matusi au kuvuruga mtiririko wa kawaida ndani ya SHAKTech143‘.
3. Kuleta hoja ambazo hazikubaliwi ndani ya SHAKTech143‘ kwa manufaa yako mwenyewe au kwa kutaka kuvuruga amani ya watumiaji wa SHAKTech143‘.
Haki ya Mali Akili
1. Haki miliki zote, nembo za biashara, haki
za usanifu, hateza na haki nyingine za mali akili (zilizosajiliwa na ambazo
hazijasaliwa) kwenye maudhui ya SHAKTech143‘ na maudhui yote (ikiwa ni pamoja
na programu) zilizoko kwenye tovuti ambazo zitaendelea kuwa mali ya SHAKTech143 au wenye leseni wengine (ambao pia ni pamoja na watumiaji wengine), vitu vifuatavyo Haviruhusiwi:-
- kunakili,
- kuchapisha upya,
- kupangua,
- kubadilisha kihandisi,
- kupakua,
- kutuma,
- kutangaza,
- kurusha au kutoa kwa umma kwa kubadiri,
au vinginevyo kutumia maudhui ya SHAKTech143‘ kwa jia yoyote isipokuwa kwa
matumizi yako binafsi na isiwe matumizi ya kibiashara au kwa matumizi mabaya au lengo baya.
2. Pia unakubali
kutokukabiliana, kubadilisha au kutengeneza kazi nyingine kutokana na maelezo
yoyote ya SHAKTech143‘ isipokuwa tu kwa matumizi yako binafsi yasiyo ya
kibiashara pia kwa masomo. Matumizi mengine yoyote ya maelezo ya SHAKTech143‘ yanahitaji
idhini rasmi ya SHAKTech143 kimaandishi.
3. Majina, picha na nembo
zinaitambulisha SHAKTech143, SHAKTech143 Media au pande nyingine na bidhaa
zao na huduma zinalindwa na hakimiliki, haki ya kubuni, na alama za SHAKTech143 Media au pande nyingine. Hakuna sehemu ya masharti haya
itakayochukuliwa kama ni kutoa leseni yoyote au haki ya kutumia alama yoyote ya
kibishara, haki ya kubuni au haki miliki ya SHAKTech143 Media
au upande mwingine wowote ule.
Michango kwa SHAKTech143
1. Kwa kubadilishana
mchango wowote (ikijumuisha maandishi yoyote yale, picha, michoro, picha za
sinema au sauti) na SHAKTech143, unaridhia kuipa SHAKTech143, kibali pasipo malipo,
idhini ya kutumia mchango huo kwa namna yoyote ile inavyotaka (ikijumuisha
kurekebisha na kubadili mchango au kuukataa mchango huo kwa sababu za kiutendaji na kiuhariri) kwa
ajili ya huduma za SHAKTech143 katika chombo chochote kile cha habari
ulimwenguni kote (ikijumuisha katika tovuti ya SHAKTech143 inayopatikana kwa
watumiaji wa kimataifa/kitaifa). Katika mazingira mengine SHAKTech143 huenda
ikabadilishana mchango wako na watu wengine au pande nyingine zinazoaminika Zaidi.
2.Hakimiliki katika mchango wako itabakia kuwa yako na idhini hii si ya kipekee,
hivyo unaweza kuendelea kutumia mchango huo katika namna yoyote ile ikiwemo
kuruhusu wengine kuutumia na pia kama ni mazuri pia hata SHAKTech143‘ wanaweza kuutumia.
3. Ili SHAKTech143 iweze kutumia mchango wako,
unathibitisha kuwa mchango wako ni kazi halisi yako mwenyewe, haidhalilishi na
haikiuki sheria zozote za Uingereza na Tanzania, kwamba unahaki ya kuipa SHAKTech143 idhini ya kutumia mchango huo kwa madhumuni maalum yaliyotajwa hapo juu, na
kwamba una ridhaa ya mtu yeyote yule anayeweza kutambulika katika mchango wako
au ridhaa ya mzazi wako au mlezi iwapo una umri wa chini ya miaka 15 au hauja barehe.
4. Kwa
kawaida tunaonyesha jina lako sambamba na mchango wako, labda uwe umeomba
vinginevyo, lakini kwa sababu za kiutendaji wakati mwingine haiwezekani
kutekeleza ombi lako. SHAKTech143 huenda ikahitaji kuwasiliana na wewe kwa
madhumuni ya kiutawala na uhakiki kuhusiana na mchango wako au kuhusiana na
miradi maalum. Kwa maelezo yote ya wakati na jinsi gani tunaweza kuwasiliana
nawe tafadhali angalia [Sera ya Faragha ya SHAKTech143] pamoja na masharti
yoyote yale katika nchi uliopo pale yanapohitajika kwa usalama zaidi.
5.Tafadhali usijihatarishe
wewe mwenyewe au wengine, kuchukua hatari yoyote ile isiyo na ulazima au kuvunja
sheria yoyote ile wakati unaandaa mchango wako ambao huenda ukabadilishana na SHAKTech143.
Hakimiliki
1. Haki miliki zote, alama za biashara, haki za kubuni
na haki nyingine zote za kazi za ubunifu (zilizosajiliwa au kutosajiliwa) ndani
na katika SHAKTech143‘ na maelezo yote (ikijumuisha matumizi yote) yaliyowekwa
katika tovuti vitabakia kuwa chini ya SHAKTech143 na au waliopewa kibali cha
leseni na SHAKTech143 (ikijumuisha watumiaji wengine). Huruhusiwi kunakili,
kutoa nakala, kuchapisha upya, kupangua, kuunda upya, kupakua, kutuma,
kutangaza, kusambaza, kuwezesha kupatikana kwa umma au vinginevyo kutumia
maelezo ya SHAKTech143‘ kwa namna ambayo ni nje ya matumizi yako binafsi,
yasiyolenga kibiashara na kuvuruga amani ya mwenzako. Pia unakubali kutokukabilina, kubadilisha au kutengeneza
kazi nyingine kutokana na maelezo yoyote ya SHAKTech143‘ isipokuwa tu kwa
matumizi yako binafsi, yasiyo ya kibiashara au kuvuruga amani ya mwenzako. Matumizi mengine yoyote ya maelezo
ya SHAKTech143‘ yanahitaji idhini rasmi ya SHAKTech143 kimaandishi.
2. Majina, picha na nembo zinaitambulisha SHAKTech143, SHAKTech143 Media au
pande nyingine na bidhaa zao na huduma zinalindwa na hakimiliki, haki ya kubuni,
na alama za SHAKTech143, SHAKTech143 Media au pande nyingine. Hakuna
sehemu ya masharti haya itakayochukuliwa kama ni kutoa leseni yoyote au haki ya
kutumia alama yoyote ya kibishara, haki ya kubuni au haki miliki ya SHAKTech143, SHAKTech143 Media au upande mwingine wowote ule. Iwapo hutaki kutoa
ruhusa kwa SHAKTech143 kulingana na masharti yaliyotajwa hapo juu, tafadhali
usiwasilishe au kubadilishana mchango wako na SHAKTech143‘.
3. Katika
tukio la mchango unaohusiana na habari tafadhali kumbuka kuwa huenda SHAKTech143 ikabadilishana na washirika au mashirika ya utangazaji
yanayo heshimika ambayo hayaruhusiwi kubadili maelezo kwa namna yoyote ile au
kuyatoa kwa mashirika mengine ya utangazaji ya Tanzania na nje ya Tanzania au ya uchapishaji.
4. Iwapo una maswali yoyote yale kuhusu maelezo ya mchango unaotolewa kwa SHAKTech143, tafadhali angalia Maelezo Yanayotokana na SHAKTech143 au Maswali Yanayoulizwa Mara kwa
Mara na Watumiaji wa SHAKTech143
5. Ili kushiriki na kutoa mchango katika sehemu
zilizochaguliwa za kijamii katika SHAKTech143‘ (ikiwemo ubao wa ujumbe na
blogs) huenda ukahitajika kujisajili. Maelezo yoyote yale ya kibinafsi
yanayotolewa kwa SHAKTech143‘ kama sehemu ya mchakato wa usajili huu au
mwiingiliano wowote ule na SHAKTech143‘ yatachukuliwa, kuhifadhiwa na kutumiwa
kulingana na sera ya faragha ya SHAKTech143. [Privacy Policy].
Kanuni za Jumuiya
Unakubali kushiriki katika jumuiya zilizopendekezwa za SHAKTech143‘
kulinga na Kanuni za Jumuiya za SHAKTech143 zilizoorodheshwa hapa chini:
1.
Kuhusu michango yako:-
1.1. Michango ni lazima iwe ya kiistaarbu na yenye mvuto.
1.2 Mwenendo wa usumbufu, kuchukiza au matusi hauruhusiwi: michango lazima iwe ya
kujenga na yenye heshima, isiwe na lengo baya au iliyotolewa kwa kusudi la
kusababisha kero.
1.3 Mchango ulio kinyume cha sheria hauruhusiwi: michango iliyo
kinyume cha sheria ni kama, usumbufu, udhalilishaji, unyanyasaji, vitisho, matusi, yenye lengo la kimapenzi, ubaguzi wa rangi, dini, ukabira au vinginevyo haikubaliki.
1.4 Uwe mvumilivu: Watumiaji wa rika zote na uwezo huenda wakaweza kushiriki katika
jumuiya husika za SHAKTech143 community.
1.5 Michango iliyo nje ya mada au yenye
lengo la uvurugaji hairuhusiwi: haturuhusu kuwasilisha mchango ambao umeshatumika
au unaofanana sana mara nyingi. Tafadhali usiwasilsilishe mchango wako kwa kutaka usikilizwe sana au kuchangia maelezo yaliyo nje ya mada
katika maeneo maalum.
1.6 Hairuhusiwi matangazo ya haina yoyote au kujitangaza.
1.7 Michango iliyo
katika lugha nyingine zaidi ya (lugha yako mfano Kiswahili na kingereza) huenda ikaondolewa
isipokuwa pale imeruhusiwa katika sheria za eneo au nchi husika.
1.8 Hairuhusiwi
kujiigiza kuwa mtu mwingine.
1.9 Hairuhusiwi majina yasiyokubalika. (mfano yenye
kuchukiza)
1.10 URLs (anuani za tovuti) zinaweza tu kutumwa au kuwasilishwa iwapo
imeruhusiwa na katika kanuni zozote zile za shirika husika.
1.11 Kutumia vibaya kwa
makusudi sehemu ya kuwasilisha malalamiko hairuhusiwi. Iwapo utaendelea kufanya
hivyo, hatua itachukuliwa dhidi ya akaunti yako.
1.12 Akaunti yako ya SHAKTech143:
Iwapo unatumia logins zaidi ya moja kwa lengo la kuivuruga jumuiya au kuwaudhi
watumiaji wengine, huenda ukachukuliwa hatua dhidi ya akaunti zako zote. Akaunti
zote lazima zisajilliwe na anwani binafsi ya barua pepe iliyo sahihi ambayo
unaitumia mara kwa mara ili barua pepe (emails) ziweze kutumwa kwako(updates).
1.13 Akaunti
zilizosajiliwa kwa kutumia anwani ya barua pepe ya mtu mwingine, au anwani ya barua pepe ya muda huenda zikafungwa pasipo kutolewa taarifa. Huenda tukahitaji
watumiaji wathibitishe tena akaunti zao iwapo tunaamini kuwa wamekuwa wakitumia
anwani ya barua pepe siyo sahihi.
1.14 SHAKTech143 ina haki ya kuzifunga akaunti
iwapo mtumiaji yeyote anaonekana kuwa anatumia wakala IPS (Internet Protocol
addresses) ili kujaribu kuficha matumizi ya akauti za SHAKTech143 zaidi ya
moja, au iwapo mtumiaji asiyemkazi wa Tanzania anajifanya kuwa ni mtumiajai wa
Tanzania, au kuvuruga huduma zetu kwa namna yoyote ile.
Usalama
Tunashauri kuwa
kamwe usitoe maelezo binasi kuhusu wewe mwenyewe au mtu mwingine yeyote yule
moja kwa moja kwa umma katika jumuiya yoyote ile ya SHAKTech143. Mahitaji ya
Kisheria: Usiwasilishe au kubadilishana mchango wowote wa kudhalilisha au ulio
kinyume cha sheria kwa namna yoyote ile katika jumuiya za SHAKTech143‘ . Hii
inajumuisha maandishi, graphics, picha za sinema, vipindi au sauti. • Maelezo ya
mchango kwa SHAKTech143‘ jumuiya yenye lengo la kufanya au kutangaza kitendo
kilicho kinyume cha sheria inapigwa marufuku vikali.
• Unakubali kuwasilisha au
kubadilishana na jumuiya za SHAKTech143‘ michango ambayo ni kazi yako halisi
tu. Usivunje, kunakili au kukiuka haki za SHAKTech143 au pande nyingine
ikiwemo hakimiliki, alama za biashara, siri za kibiashra, faragha, kujitangaza,
mtu binafsi au haki za wamiliki. Iwapo Una Umri Chini ya Miaka 16:
• Tafadhali
pata idhini ya mzazi au mlezi kabla hujashiriki katika jumuiya zozote zile za SHAKTech143‘.
• Kamwe usitoe maelezo binafsi kuhusu wewe mwenyewe au mtu
mwingine yeyote yule (kwa mfano shule, namba ya simu, jina lako kamili, anwani
ya nyumbani au anwani ya barua pepe) yaani utambulisho wako kiujumla.
Iwapo Utakiuka Kanuni Hizi za Jumuiya:
Iwapo utakaidi kufuata kanuni hizi za Jumuiya (na/au zinginezo tofauti katika
shirika la eneo husika) wakati unashiriki katika SHAKTech143‘ jumuiya ya SHAKTech143 itakutumia ujumbe wa barua pepe unaokufahamisha kwanini mchango wako umekataliwa
au kuhaririwa. Ujumbe huu utajumuisha pia onyo kuwa kuendelea kukiuka kanuni
hizi kunaweza kusababisha hatua kuchukuliwa dhidi ya akaunti yako au zako. Hatua
hii huenda ikajumuisha mchango wowote uliotumwa na wewe kuangaliwa kabla ya
kuruhusiwa kwenda katika tovuti au kusitishwa kwa muda au moja kwa moja uwezo
wako wa kushiriki katika eneo au maeneo yoyote ya jumuiya za SHAKTech143‘ .
Iwapo utawasilisha au kubadilishana mchango wenye kukera au usiokubalika au
na jumuiya zozote zile za SHAKTech143‘ au popote pale katika SHAKTech143‘ au
vinginevyo kujihusisha katika mwenendo wowote ule wa kuvuruga amani katika SHAKTech143‘ , na SHAKTech143 inafikiria athari za mwenendo kama huo kuwa kubwa au
kurudiwa tena, SHAKTech143 huenda ikatumia maelezo yoyote yale yanayopatikana
kuzuia ukiukwaji zaidi kutokea. Hii inaweza kuwa ni pamoja na kuzifahamisha
pande nyingine kama vile mwajiri, shule au mtoa huduma ya email kuhusu ukiukaji
huo. SHAKTech143 ina haki ya kufuta mchango wowote ule,au kuchukua hatua dhidi
ya akaunti yoyote ile ya SHAKTech143, wakati wowote, kwa sababu yoyote ile.
Kukana na Kupunguza Wigo wa Uwajibikaji
15. Sehemu kubwa ya mchango unaotumwa katika jumuiya za SHAKTech143‘ inafanywa na umma. Maoni yanayotolewa ni ya
kwao na isipokuwa pale imeelezwa vinginevyo maoni hayo si ya SHAKTech143 au SHAKTech143 Media. SHAKTech143 na SHAKTech143 Media haihusiki na mchango
wa maelezo yoyote yaliyotumwa na umma katika SHAKTech143‘ au kwa upatikanaji
wake au mchango wa tovuti za upande mwingine wowote ule zinazopatikana
kupitia SHAKTech143‘ . Viunganishi vyovyote vile kwa upande mwingine wa tovuti
kutoka SHAKTech143‘ haimaanishi tovuti hiyo imeidhinishwa na SHAKTech143 au SHAKTech143 Media na matumizi yoyote ya tovuti hiyo ni kwa athari yako
mwenyewe.
16.Hakuna kitu chochote
katika masharti haya kinachoiondoleaSHAKTech143 uwajibikaji au lawama juu ya upotevu au maumivu yanayosababishwa na uzembe wake uliothibitibitika. Kwa mujibu wa
sentensi iliyotangulia,SHAKTech143 naSHAKTech143 Media haitawajibika kwa
upotevu wowote ule au uharibifu ufuatao (iwe uharibifu huo au upotevu huo ulitabirika, kujulikana au vinginevyo):
(a) kupotea kwa data;
(b) kupotea kwa
mapato au faida iliyotarajiwa; (c) kupotea kwa biashara;
(d) kupotea kwa nafasi;
(e) kupotea kwa nia njema au kuathirika kwa hadhi;
(f) upotevu ulizoziathiri
pande nyingine; au
(g) matokeo au athari yoyote ile isiyo ya moja kwa moja
maalum au uharibifu unaotokana na matumizi ya SHAKTech143‘ bila kujali
kuchukuliwa hatua.
17.SHAKTech143 naSHAKTech143 Media haitoi hakikisho kuwa
ufanyaji kazi unaopatikana katika SHAKTech143‘ hautaingiliwa au kutokuwa na
makosa, kwamba makosa yatarekebishwa, au kwamba SHAKTech143‘ au seva
inayowezesha upatikani wake haiwezi kuwa na virusi. Unakubali kuwa ni wajibu
wako kutumia utaratibu unaohitajika na kukagua virusi (ikiwemo kipinga virusi na
ukaguzi mwingine wa kiusalama) kutosheleza mahitaji yako maalum kwa usahihi wa
data zinazoingia na kutoka.
18.Kushindwa au kuchelewa kwa SHAKTech143
kutekeleza au kusimamia yoyote kati ya masharti haya haiiondolei SHAKTech143
haki hiyo.
Dhima
Kwa kupakua na kusanikisha programu za SHAKTech143 zinazoweza
kufutikwa (“Dhima ya SHAKTech143”) na kutumia kuonyesha maudhui ya SHAKTech143 (“Maudhui ya SHAKTech143”) kwenye kompyuta yako unakubaliana na masharti yaliyoainishwa hapo chini. Masharti ya Dhima
3. Waranti & Uwajibikaji
3.1 Dhima za
SHAKTech143 na Maudhui ya SHAKTech143 zinaundwa kwa msingi wa “kama zilivyo”
na “kama zinavyopatikana” na unapakua, kusanikisha na kutumia Dhima za SHAKTech143
na kuangalia Maudhui ya SHAKTech143 kwa utashi na madhila yako.
3.2
SHAKTech143 imechukua tahadhari kuhakikisha kuwa Dhima za SHAKTech143 Widget
na Maudhui ya SHAKTech143 kuepusha upungufu, makosa, virusi au hitilafu, hata
hivyo SHAKTech143 haisemi kila kitu kitafanya kazi bila matatizo.
3.3 Kadri
inavyoruhusiwa kisheria, SHAKTech143 haitoi kisio la aina yoyote
(lidhaniwalo, lazima au vinginevyo) kuhusiana na Dhima ya SHAKTech143, Maudhui
ya SHAKTech143 au tovuti ya SHAKTech143 na SHAKTech143 haitahusika kwa
hasara yoyote au uharibifu utakaotokana au kuhusishwa na Dhima ya SHAKTech143
au Maudhui ya SHAKTech143.
3.4 Unashauriwa kuchukua tahadhari zote kulinda
kompyuta yako isiambukizwe virusi.
3.5 SHAKTech143 inaweza kubadilisha Maudhui
ya SHAKTech143 kwa utashi wake na inaweza kuzuia matumizi ya Dhima ya SHAKTech143 endapo utakiuka Sheria hizi za Mtumiaji wa Mwisho.
3.6 Iwapo
masharti yoyote katika haya yanaonekana kuwa ni kinyume cha sheria, batili au
vinginevyo hayawezekani kutekelezeka kutokana na sababu za kisheria katika nchi
au jimbo lolote lile ambako masharti haya yamelengwa kufanya kazi, basi kwa
kiwango na ndani ya uwezo wa kisheria ambako masharti hayo ni kinyume na sheria,
batili au hayatekelezeki, yatafutwa kutoka katika masharti haya na masharti
yaliyobaki yataendelea kuwepo na kutumika.
3.7 Kushindwa au kuchelewa kwa SHAKTech143 kufanyia kazi au kutekeleza haki yoyote ile katika masharti haya haiondolei
SHAKTech143 haki ya kutekeleza haki hiyo.
3.8 Matumizi ya tovuti ya [SHAKTech143‘] yanahusishwa na masharti na kanuni za Tanzania , ambayo ni lazima
yatafsiriwe kulingana na sheria ya Tanzania na kuhusishwa chini ya uwezo wa
kipekee wa kimahakama katika mahakama za Kitanzania.
Hitimisho
Iwapo una maswali
maalum kuhusu Masharti ya Matumizi haya, tafadhali tuma ujumbe wa barua pepe
email kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano hapo chini.