Jinsi ya Kutumia Telegram Bure Tanzania Bila VPN au Proxy Kwa Plus Messenger (Beta)
Watumiaji wengi wa Telegram hapa Tanzania wanatafuta njia rahisi ya kutumia app hii bila kutumia VPN au Proxy. Kwenye makala hii ya SHAKTech143, nitakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kutumia Telegram bure kwa kutumia Plus Messenger (Beta), jinsi ya kuipata, kujisajili pamoja na faida na hasara zake.
Plus Messenger (Beta) Ni Nini?
Plus Messenger (Beta) ni toleo maalum (modified version) la Telegram lenye vipengele vya ziada kama:
- Custom themes (kubadilisha muonekano wa app)
- Privacy settings za ziada
- Kuficha chats maalum
- Control ya tabs na categories
- Muonekano wa kipekee na wa kisasa
App hii hutumia mfumo ule ule wa Telegram lakini inaongezewa features zaidi.
Jinsi ya Kupata Plus Messenger (Beta)
- Fungua Google Play Store na tafuta Plus Messenger au bonyeza hapa.
- Unaweza kuipata pia sehemu nyingine ila ziwe salama
- Pakua app na uisakinishe kwenye simu yako.
- Ruhusu permissions zote muhimu wakati wa kusakinisha.
Tahadhari: Usipakue APK kutoka website zisizoaminika ili kuepuka virusi au malware.
Jinsi ya Kujisajili au Login
- Fungua Plus Messenger (Beta)
- Bonyeza Start Messaging
- Weka namba yako ya simu na chagua code ya Tanzania (mfano: +255...)
- Subiri SMS ya verification
- Weka code uliyopewa
- Maliza kuweka jina na profile picture (hiari)
- Kama una tayari account telegram uta login kawaida ila code utatumiwa telegram ulipo login kwa huo wakati.
Baada ya hapo akaunti yako itafunguka kama Telegram ya kawaida.
Je ni yapi maoni kwa watumiaji wa plus messenger
Baadhi ya watumiaji wameripoti kuwa Plus Messenger (Beta) wakati mwingine:
- Inafanya kazi bila VPN au proxy
- Inatumia data kidogo sana
- Inaweza kuruhusu kutuma na kupokea meseji hata bila bando kamili
Hata hivyo, hii hutegemea:
- Mtandao unaotumia (Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel n.k.)
- Muda na mabadiliko ya mfumo wa mtandao
- Version ya app unayotumia
Kumbuka: Hakuna guarantee ya 100% kuwa itakuwa bure muda wote.
Faida za Kutumia Plus Messenger (Beta)
- Muonekano mzuri na customizable
- Privacy settings nyingi zaidi
- Unaweza kupanga chats kwa categories
- Ina features nyingi kuliko Telegram ya kawaida
- Wakati mwingine inafanya kazi kwa kuitaji msaada kidogo wa VPN ao proxy
Hasara za Kutumia Plus Messenger
- Si app rasmi ya Telegram
- Inaweza kuacha kufanya kazi muda wowote
- Inaweza kuwa na hatari ya usalama kama chanzo si rasmi
- Akaunti inaweza kuwa kwenye risk kama Telegram watazuia mod apps
- Huwezi kulipia chochote au kununua star ⭐
Je, Ni Salama Kutumia?
Kimsingi Plus Messenger hutumia mfumo wa Telegram, lakini kwa sababu si official app, inashauriwa:
- Usitumie kwa taarifa nyeti sana
- Pakua kutoka chanzo kinachoaminika
- Fanya update mara kwa mara
- Uwe makini na ruhusa (permissions) unazotoa
Hitimisho
Kama unatafuta njia mbadala ya kutumia Telegram bila VPN au Proxy hapa Tanzania, basi Plus Messenger (Beta) inaweza kuwa chaguo la kujaribu na unajisajili bule hakuna malipo. Hata hivyo, tumia kwa tahadhari kwani hali inaweza kubadilika muda wowote kulingana na mtoa huduma wa mtandao au sera za Telegram.
Endelea kufuatilia SHAKTech143 kwa tips zaidi za teknolojia na internet tricks za kisasa.

Asante sana imekubali ila naona mpaka proxy
ReplyDelete